Queen Darleen na Zuchu kuja na Collabo.
Joyce Shedrack
November 5, 2024
Share :
'First Lady wa muziki lebo ya Wasafi #wcbwasafi na dada wa kambo wa Msanii wa Bongofleva #diamondplatnumz Queen Darleen jana ilikuwa ni siku ya mfanano na siku ya kuzaliwa kwake ambapo kupitia 'Insta story' ya msanii #zuchu katika kumtakia kheri kwenye siku ya kuzaliwa kwake aliwasanua pia mashabiki kuwa ngoma ya pamoja ya wadada hao kutokaea #wcbwasafi ipo tayari akimuuliza @queendarleen_ kazi hiyo itoke lini.
Queen Darleen bado ni msanii aliyesaini chini ya lebo ya @wcb_wasafi na kupitia ukurasa wa Instagram wa lebo hiyo pia walimtakia kheri na kuweka wazi kwamba mashabiki wakae mkao wa kula kwani hivi karibuni atakuja kwa ujio mpya.
Queen Darleen aliacha kwa mda musuala ya mziki na anatarajiwa kurejea hivi karibuni, Je maoni yako ni yapi juu ya ujio wake.