pmbet

Rachid kuondoka mwisho wa msimu Azam

Sisti Herman

June 11, 2025
Share :

 

Ripoti za usajili zinaonyesha kuwa Kocha Rachid Toussi wa Azam FC ataondoka mwisho wa msimu huu, na timu hiyo ilishafanya maamuzi ya kumuacha na tayari kocha Rachid Toussi anajua, Azam FC wamemwambia amalize mechi mbili za mwisho za ligi kuu ya NBC zilizobaki.

Azam FC itaachana na Kocha Rachid Toussi mwishoni mwa msimu huu, Rachid Toussi ataondoka pamoja na wasaidizi wake Badr Driss, kocha wa viungo Ouajou Driss na kocha wa makipa Rachid El Mekkaoui.

Kocha Rachid Toussi na wenzake walisaini mkataba wa mwaka mmoja September 07, 2024, Azam FC kwasasa ipo kwenye mchakato wa kutafuta Kocha mpya.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet