Radi yaua 6 ikiharibu sherehe na kuua
Eric Buyanza
December 5, 2023
Share :
Watu sita wamefariki dunia na watano wamejeruhiwa kwa kupigwa na radi wakiwa katika sherehe za kumpongeza kijana aliyemaliza kidato cha nne.
Tukio hilo limetokea jana Desemba 3, 2023 majira ya saa 12 jioni katika Kijiji cha Maparagwe Kata ya Chikukwe Wilaya ya Masasi.
Watu hao walikutwa na maafa hayo wakiwa kwenye sherehe ya kumpongeza kijana wao aliyehitimu kidato cha nne nyumbani kwao, ambapo mvua ilianza kunyesha ikiambatana na radi.