Rafu ya Messi yazua mjadala, wanauliza kwanini hakupewa kadi?
Eric Buyanza
June 17, 2026
Share :
Lionel Messi amenusurika kupewa kadi nyekundu kwenye Kombe la Dunia baada ya faulo yake mbaya wakati Argentina iliposhinda 3-0 dhidi ya Algeria.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 38 alikuwa katika kiwango bora zaidi huku mabao yake matatu (hat-trick) yakiwapa ushindi mabingwa hao watetezi wa Kombe la Dunia katika mchezo wao wa ufunguzi wa Kundi J.
Tukio hilo lilitokea baada ya bao la kwanza la Messi huku akiionekana kukabana na nahodha wa Algeria Aissa Mandi ndipo alipomkanyaga eneo la kiazi cha mguu na kushuka kwenye kisigino.
Refa wa Poland, Szymon Marciniak, aliizawadia Algeria mkwaju wa faulo lakini Messi hakupokea hata kadi ya njano.






