Raheem Sterling akumbwa na tuhuma za madawa ya kulevya.
Joyce Shedrack
May 30, 2026
Share :
Mshambuliaji wa zamani wa Man City,Arsenal na Chelsea anayeichezea Feyenoord amekamatwa baada ya ajali iliyohusisha gari lake la Lamborghini kwenye barabara kuu ya M3 alfajiri ya Alhamisi, Nchini Uingereza huku akituhumiwa kwa utumiaji wa madawa ya kulevya.

Polisi wa Hampshire wamethibiisha tukio hilo na kuweka hadharani tuhumu zinazomkabili mchezaji huyo ambaye kwa sasa ameachiliwa kwa dhamana.
“Muda mfupi kabla ya saa 3:00 asubuhi Alhamisi, tulipokea taarifa kwamba gari aina ya Lamborghini lilikuwa limegonga vizuizi vya barabara kwenye upande wa kusini wa M3, karibu na Minley Interchange. Hakuna gari lingine lililohusika na hakuna majeruhi walioripotiwa.”
“Dereva huyo, mwanaume mwenye umri wa miaka 31 kutoka Berkshire, amekamatwa kwa tuhuma za kuendesha gari akiwa chini ya athari za dawa za kulevya, kuendesha gari kwa hatari, kumiliki dawa ya kulevya ya Daraja C, na kushindwa kutoa sampuli inayohitajika kwa uchunguzi. Ameachiwa kwa dhamana huku uchunguzi wetu”Imesema taarifa ya Jeshi la Polisi.





