Raia wa Comoro adakwa na aina mpya za dawa za Kulevya
Sisti Herman
April 4, 2024
Share :
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imemkamata Ahmed Bakar Abdou (32), raia wa Comoro akiwa na kilogramu 4.623 za aina mpya ya dawa za kulevya inayoelezwa kusababisha madhara ya haraka kwa mtumiaji.
Dawa hizo zinayofahamika kama Methylene Dioxy Pyrovalerone (MDPV), zimekutwa kwa mtuhumiwa huyo akiwa katika harakati za kuzisafirisha kutokea Dar es Salaam.
Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Aprili 4, 2024 na Kamishna Jenerali wa DCEA , Aretas Lyimo inaeleza kuwa MDPV ni dawa mpya ya kulevya iliyo katika kundi la vichangamshi inayotengenezwa kwa kutumia kemikali bashirifu.
“Dawa hii ina kemikali inayoweza kuleta madhara ya haraka kwa mtumiaji ikilinganishwa na dawa nyingine za kulevya. Pia, imeongezwa nguvu ya kilevi inayozidi cocaine, heroin na methamphetamine.
“Pia, dawa hii ya kulevya huuzwa kwa njija ya mtandao (internet) na husafirishwa kupitia kampuni za usafirishaji vifurushi na hufichwa kwa kuwekwa chapa za majina bandia kama vile bath salts, Ivory Wave, plant fertilizer, Vanilla Sky, na Energy,” amesema Kamishna Lyimo.