pmbet

Raia wa kigeni akamatwa akitorosha Almasi za Bilioni 1.7

Sisti Herman

May 25, 2025
Share :

Almasi zenye thamani ya zaidi ya Dola za kimarekani 635,000 sawa na Sh.bilioni 1.7 zimekamatwa zikisafirishwa kinyume na utaratibu katika uwanja wa ndege wa Mwanza.
 


Akithibitisha kukamatwa kwa madini hayo usiku wa kuamkia leo Mei 24 katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Waziri wa Madini Antony Mavunde amesema yalikamatwa Mei 18 yakisafirishwa katika mabegi manne na raia wa kigeni.

"Majira ya saa saba mchana maofisa usalama kwa kushiriana na Mamlaka husika walibaini utoroshwaji almasi hiyo yenye uzito wa karati 2729.82 yenye thamani ya Dola ya kimarekani 635,847.66 Sawa na Sh.bilioni 1.745,"

"...yakiwa yamefichwa kwenye mabegi manne na raia mwenye asili ya India kwa lengo la kuyasafirisha bila vibali halali wala kufuata taratibu za kisheria," amesema Mavunde.

Mavunde amesema Wizara imesikitishwa na tukio hilo la utoroshwaji wa rasilimali za Taifa na kuwa inalaani vikali vitendo vya namna hiyo.

"Ikumbukwe kuwa utoroshwaji wa madini ni kosa la jinai unaoikosesha Nchi mapato na kudhohofisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa ujumla," amesema Mavunde.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet