Raia waandamana kisa umeme kukatika
Sisti Herman
June 9, 2024
Share :
Mamia ya raia wa Ghana walifanya maandamano katika Mji Mkuu wa Accra jana kupinga kukatika kwa Umeme kunakoathiri biashara na maisha ya kila siku katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.
“Hakuna taa, hakuna wateja tunapaswa kupata riziki gani?” aliuliza Kwame Danso, Mfanyakazi wa ndani wa kutengeneza nywele, akiinua bango lililosomeka hivi: “Simamisha kukata umeme, okoa kazi zetu.
Waandamanaji hao, wakiwa wameshikilia taa zinazotumia mafuta ya taa kuashiria masaibu yao na kuungwa mkono na watu mashuhuri wa eneo hilo, waliitaka Serikali kuleta utulivu wa usambazaji wa umeme.
Ingawa ni mojawapo ya nchi za Kiafrika zilizoendelea zaidi katika uwekezaji wa umeme, Ghana inakabiliwa na uhaba wa kudumu huku ikijitahidi kuinua uwezo wake wa uzalishaji ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka.
Umeme umekuwa suala kuu la kampeni katika nchi hii yenye utajiri wa dhahabu na mafuta katika maandalizi ya Uchaguzi uliopangwa kufanyika Desemba.