pmbet

Raia wakiwemo watoto, watakiwa kujiunga na M23 kwa lazima

Eric Buyanza

June 11, 2026
Share :

Shirika la Human Rights Watch inawashutumu waasi wa M23 kwa kulazimisha raia wa DR Congo kujiunga na kundi hilo la kijeshi kwa lazima.

 

Ripoti ya shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch, imesema kundi la waasi la  M23 linaloungwa mkono na Rwanda, limewalazimisha maelfu ya watu kujiunga na kundi hilo mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, na kuwashikilia katika mazingira yasiyokuwa ya kibinadamu.

 

Ripoti hiyo iliyochapishwa jana Jumatano imebainisha kwamba maelfu ya wanajeshi wa Kongo, wanachama wa makundi ya wanamgambo na raia wamekuwa wakizuiliwa na kundi hilo.
 

Baadhi ya wanaoshikiliwa ni pamoja na watoto  wa chini ya umri wa miaka 12 ambao wamepelekwa kwenye vituo au makambi ya mafunzo ya kijeshi ambako wamekuwa wakishikiliwa chini ya mazingira mabaya kwa wiki au miezi kadhaa wakipitia ukatili wa kupigwa na hata mauaji.
 

Ripoti hiyo ya Human Rights Watch imetokana na mahojiano yaliyofanyiwa wafungwa 102 wa zamani waliokuwa chini ya kundi hilo la M23.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet