Raila awasifu Polisi wa Tanzania, awakataa wa Kenya
Sisti Herman
July 8, 2025
Share :
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga ameonekana kuwakashifu polisi wa Kenya kwa kusema, "Tulirithi jeshi la polisi kutoka kwa wakoloni. Linapaswa kufanyiwa mageuzi ili liwe chombo cha kuhudumia wananchi. Huko Tanzania, polisi ni wenye urafiki na hawapendi kutumia risasi ovyo."
Odinga, ametoa wito wa kufanyika kwa mageuzi ya haraka katika jeshi la polisi ili kukomesha kuzorota kwa uhusiano kati ya polisi na raia, jambo ambalo linazua wasiwasi.