pmbet

Rais achunguzwa kwa kufanya operesheni ya 'Urembo wa pua'

Eric Buyanza

December 6, 2024
Share :

Ofisi ya Mwendesha mashitaka mkuu nchini Peru inaanzisha uchunguzi dhidi ya Rais wa nchi hiyo Dina Boluarte anayetuhumiwa kukwepa majukumu yake.

Uchunguzi huo unakuja baada ya kuibuka kwa kashfa ya kiongozi huyo kutoonekana hadharani mwezi Juni na Julai mwaka jana, akiwa amejipa likizo baada ya kufanyiwa operesheni ya pua.

Katika siku za karibuni kulizuka uvumi kwenye mitandao ya kijamii nchini Peru kwamba rais huyo alitumia muda wa kazi kufanya operesheni ya urembo wa pua yake.

Hata hivyo siku ya Jumanne, Waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo, Alberto Otarola, alimtetea Rais huyo kwa kuiambia kamati ya Bunge kwamba Rais Boluarte aliwahi kumwambia kwamba anakwenda kufanyiwa operesheni ya pua kutokana na shida ya kupumua.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet