Rais afuta posho za Mawaziri
Sisti Herman
July 15, 2025
Share :
Rais wa Ghana John Mahama ametoa agizo la kufuta malipo ya posho za mafuta kwa wote walioteuliwa kisiasa.
Wanaotarajiwa kuathiriwa na agizo hilo ni pamoja na mawaziri na wakuu wa taasisi za umma waliochaguliwa na rais.
Serikali yake imesema huu ni mpango wa serikali wa kupunguza gharama na kuelekeza fedha za umma katika maeneo ya kipaumbele.