Rais Al Nassr aliyemchukulia poa Ronaldo kutimuliwa
Sisti Herman
February 11, 2026
Share :

Rais wa klabu ya Al-Nassr, Abdullah Al Majid, anatarajiwa kuondolewa kwenye nafasi yake hivi karibuni. Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo ya Saudi Arabia zinaashiria kuwa mabadiliko ya uongozi yanakaribia, huku kukiwa na shinikizo la kuboresha usimamizi wa timu hiyo inayojivunia mastaa kama Cristiano Ronaldo.
Rais huyo wiki iliyopita akichagiza maoni yake kuhusu mgomo wa Rovaldo kuhusu amsuala tofauti yanayohusiana na usimamizi wa timu hiyo alinukuliwa akisema "yeye ni muhimu kuliko Ronaldo" kwenye timu hiyo.
Ingawa sababu rasmi hazijawekwa wazi na Al-Nassr FC, inaaminika kuwa bodi ya wakurugenzi inatafuta mwelekeo mpya ili kufikia malengo ya klabu hiyo katika ligi ya Saudi Pro League.





