Rais aliyempiga refa afungiwa maisha
Sisti Herman
December 15, 2023
Share :
Aliyekuwa Rais wa klabu ya soka ya MKE Ankaragucu ya nchini Uturuki, Faruk Koca amefungiwa maisha kujihusisha na masuala ya soka baada ya kumpiga ngumi mwamuzi mwishoni mwa mechi dhidi ya Caykur Rizespor ambapo mechi iliisha kwa sare ya 1-1.
Shirikisho la Soka la Uturuki (TFF) limefikia uamuzi huo wa kumfungia Faruk Koca huku klabu ya MKE Ankaragucu ikipewa adhabu ya kulipa faini ya lira milioni mbili (£54,000) sawa na zaidi ya milioni 149 za Kitanzania.
Timu hiyo pia imetakiwa kucheza michezo mitano ya nyumbani bila mashabiki kutokana na machafuko hayo yaliyohusisha mashabiki na viongozi wa klabu.