Rais awachimba mkwara Mawaziri wanaosinzia kwenye Vikao
Sisti Herman
April 3, 2025
Share :
Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema ametoa onyo kali kwa mawaziri wake wenye tabia ya kusinzia vikaoni.
Akizungumza wakati wa kumuapisha Waziri wa Serikali za Mitaa, Gift Sialubalo, Rais Hichilema alionesha kuchukizwa na mawaziri ‘wanaochapa usingizi’ wakati wa vikao na kushindwa kutoa maamuzi muhimu kwa maendeleo ya nchi hiyo.
Rais huyo amesema tukio hilo ni uhalifu.