pmbet

Rais Burkina Faso awachimba mkwara 'Mabeberu'

Sisti Herman

January 3, 2025
Share :

 

 

Akihutubia katika hotuba yake ya kuufunga mwaka 2024, Rais mdogo zaidi barani Afrika (36), Kapteni Ibrahim Traoré, kutoka nchini Burkina Faso amesema kuwa mwaka mpya 2025 ''taifa lake halitaendeshwa kwa msaada wa nchi za kigeni" huku akisisitiza kuwa utakuwa ni mwaka wa kupata uhuru kamili au kifo.

Kiongozi huyo kijana alisema kuwa mwaka 2025 maadui wasitegemee kuona taifa lake likiwaangukia chini ya miguu yao kuomba msaada. ingawa hakuwataja maadui hao kwa majina rasmi.

Traoré alisema “....Tumekuwa wahanga kwa sababu ya utajiri tulionao ambao mabeberu wanataka kuuchukua kwa gharama zozote zile na kuendelea kutuweka kwenye utumwa.. Hatutakubali tunaenda kulinda mali zetu. Burkina Faso haitakata tamaa. Burkina Faso haitasalimu amri. Burkina Faso itapambana nao”

 

"Tunajivunia kupambana kama wanajeshi vitani na kurudisha utu wa watu wetu na tutaendelea kufanya hivyo. Wale wenye ndoto ya kuona Burkina Faso ikiwa chini ya magoti yao ikihangaika kutafuta pumzi wanapaswa kujua kuwa wameshindwa, kwa sababu wale walio hatarisha maisha jana wametufundisha kuendelea kupambana hadi tutakapo pata uhuru wetu kamili. Mungu aufanye mwaka 2025 kuwa mwaka wetu wa ushindi wa mwisho dhidi ya adui zetu. Ahsanteni nyote. Ardhi au Kifo!. Tutashinda !."

 

Hizo ni nukuu za Kapteni Ibrahim Traoré, Rais wa mpito wa Burkina Faso, Novemba 10, 2024.

Wachambuzi wanasema kuwa mwaka 2025 huenda bara la Afrika likashuhudia kutangazwa kwa uhuru wa awamu ya pili ya taifa hilo la Afrika magharibi (Second Phase of Independence) baada ya ule wa kwanza ambao waliupata kutoka kwa Ufaransa kwenye miaka ya [1960>].

Hivi karibuni imeshuhudiwa kiongozi huyo akizindua miradi mikubwa ya kimkakati kama viwanda viwili vya usindikaji wa nyanya, viwanda vya kuchakata dhahabu ghafi ili kuzuia usafirishaji wa madini kwenda nje ikiwa ni pamoja na kuyafutia makampuni ya nje leseni ya kuchimba madini akidai kuwa yapo kwaajili ya kupora rasilimali za wananchi wa Burkina Faso.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet