Rais Burundi aliyezikwa Mali kufukuliwa na kuzikwa Burundi
Sisti Herman
July 11, 2024
Share :
Ikiwa ni miaka minne tangu kufariki nchini Ufaransa na kuzikwa nchini Mali alipokuwa mwakilishi wa Umoja wa mataifa, Mwili wa Aliyekuwa Rais wa Burundi Pierre Biyoya unatarajiwa kufukuliwa na kusafirishwa kisha kuzikwa kwa heshima nchini kwake Burundi.
Pierre Buyoya aliyefariki Desemba 17,2020 Mwili wake utapelekwa nchini Burundi Julai 14,2024 kwa ajili ya kuzikwa kwa heshima zoezi litakalofanyika tarehe 17 Julai mwaka huu.
Pierre Buyoya aliingia madarakani katika nyakati mbili tofauti, mwaka wa 1987-1993 na 1996 hadi mwaka wa 2003.