Rais Félix Tshisekedi amfuta kazi Mkuu wa majeshi
Eric Buyanza
December 20, 2024
Share :

Wakati hali ya usalama ikiendelea kuzorota huku waasi wa M23 wakiendelea kusonga mbele mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo haswa katika eneo la Lubero, Rais wa nchi hiyo Félix Tshisekedi amemfuta kazi Mkuu wa Majeshi Jenerali Christian Tshiwewe Songesha.
Jenerali Tshiwewe anaondoka baada ya kushikilia nafasi hiyo kwa miaka miwili, nafasi yake imechukuliwa na Jenerali Banza Mwilambwe Jules.
Kabla ya kupandishwa cheo, Luteni Jenerali Banza Mwilambwe Jules alikuwa akihudumu kama naibu mkuu wa masuala ya kijeshi katika ofisi ya rais. Banza ni mmoja ya watu wanaoaminiwa sana na Rais Tshisekedi.
👉RFI





