pmbet

Rais FFF kushindana na Infantino Urais FIFA

Sisti Herman

November 17, 2026
Share :

 

Rais wa Shirikisho la Soka la Ufaransa (FFF), Philippe Diallo, amekubali kugombea dhidi ya Gianni Infantino.

Vyama vya soka vya mataifa ya Ulaya, ambavyo vina uwakilishi katika Kamati Tendaji ya UEFA, vimemuunga mkono kwa kauli moja.

 

Mgombea huyo, Diallo, sasa anatarajiwa kuidhinishwa rasmi na Kamati Tendaji ya FFF katika kikao kitakachofanyika kesho.

 

Katika kikao kilichofanyika leo chini ya uenyekiti wa Rais wa UEFA, Aleksander Čeferin, vyama vya soka vya mataifa hayo vilivyopo kwenye Kamati Tendaji ya UEFA vilimwalika Diallo kugombea nafasi hiyo.

 

UEFA inasema kuwa Diallo ana “uzoefu mpana katika ngazi zote za mchezo huo; amewahi kuongoza shirika linalowakilisha klabu za soka za kulipwa nchini Ufaransa, kuhudumu katika bodi ya ligi ya kulipwa ya Ufaransa, na kufanya kazi ndani ya mifumo ya FIFA ya utatuzi wa migogoro, kabla ya kuwa Rais wa FFF na mjumbe wa Kamati Tendaji ya UEFA mwaka 2023.”

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet