pmbet

Rais FIFA aipongeza Yanga

Sisti Herman

June 5, 2024
Share :

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), Gianni Infantino ametuma salamu za pongezi kwa Mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC 2023/2024 Klabu ya Young Africans.

Infantino amesema juhudi zao katika msimu mzima zimezaa matunda na kupata taji hilo muhimu huku akiwapongeza wanachama wote wa Klabu hiyo kwa mafanikio hayo.

Aidha amemshukuru Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia kwa kazi nzuri na kujitolea kwa maendeleo ya mpira wa miguu wa Tanzania.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet