pmbet

Rais Iran: Hatutakubali kutishiwa na Marekani

Sisti Herman

September 24, 2026
Share :

 

Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, amesema Iran haitawahi “kupiga magoti” baada ya karibu miezi saba ya vita dhidi ya Marekani na Israel, huku akisisitiza kuwa Tehran iko tayari kufikia suluhisho la kidiplomasia la mzozo huo.

Akijibu tishio la Rais wa Marekani, Donald Trump, kwamba Jamhuri ya Kiislamu inaweza “kuangamizwa kabisa” iwapo makubaliano hayatapatikana hivi karibuni, Pezeshkian aliliambia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa:“Upinzani wa wananchi wa Iran utaongezeka zaidi mbele ya vikwazo, kuongezwa kwa shinikizo na vitisho.”

Pezeshkian pia amesisitiza kuwa makubaliano yoyote lazima yajumuishe kusitishwa kwa kile Iran inachokitaja kuwa ni kizuizi cha Marekani kinachozuia meli za Iran kutumia njia muhimu ya majini katika Ghuba.

“Haikubaliki kwamba kila mtu anufaike na Mlango-Bahari wa Hormuz, huku sisi tukinyimwa fursa ya kuutumia,” amesema.

Hakukuwa na tamko la haraka kutoka upande wa Marekani, ambao ujumbe wake ulitoka katika ukumbi wa baraza kuu mwanzoni mwa hotuba ya Pezeshkian.

Chanzo BBC News

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet