Rais Korea aliyewapa nchi wanajeshi apingwa na Wabunge
Sisti Herman
December 4, 2024
Share :
Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol ametangaza kuwa ameondoa sheria ya kijeshi nchini Korea Kusini, saa chache baada ya kuitangaza.
Hatua hiyo inawadia baada ya wabunge 190 waliokuwepo Bungeni mjini Seoul kwa kauli moja kuzuia hatua hiyo.
Rais wa Korea Kusini alisema: "Baada ya Bunge la Kitaifa kutaka kuondoa sheria za kijeshi, wanajeshi wa sheria za kijeshi wameondolewa.
"Nitakubali ombi la Bunge la Kitaifa na kuondoa sheria ya kijeshi kupitia mkutano wa baraza la mawaziri."
Wakati huo huo, chama kikuu cha upinzani nchini Korea Kusini kimemtaka rais wa taifa hilo, Yoon Suk Yeol kujiuzulu ama apigiwe kura ya kutokuwa na imani naye kutokana na hatua yake ya kutangaza sheria ya kijeshi katika taifa linaloamini demokrasia.
Mmoja wa wanachama waandamizi wa chama cha upinzani cha Democratic Party amesema ilibainika tangu awali kwamba Yoon hawezi kuendesha nchi hiyo kwa njia za kawaida.
Katika hotuba yake Jumanne usiku, alielezea majaribio ya upinzani wa kisiasa kuhujumu serikali yake kabla ya kusema kwamba ametangaza sheria ya kijeshi "kukandamiza vikosi vinavyopinga serikali ambavyo vimekuwa vikisababisha uharibifu".
Baadhi ya watu waliozungumzia kutangazwa kwa sheria hiyo walielezea namna walivyochanganyikiwa na tangazo hilo.