Rais Paul Biya azua Gumzo kutoonekana hadharani kwa zaidi ya siku 53
Sisti Herman
August 4, 2026
Share :

Rais Paul Biya yuko wapi? ni swali lililogonga vichwa vya habari baada ya Kutoonekana hadharani kwa kiongozi huyo mkuu wa nchi ya Cameroon mwenye umri mkubwa zaidi duniani kwa muda wa rekodi ya siku 53 kumeibua tena uvumi nchini mwake, Cameroon, kuhusu iwapo yu hai au amefariki dunia, licha ya kuwa kujadili hali yake ya afya ni kinyume cha sheria nchini humo.
Paul Biya hajaonekana hadharani tangu tarehe 7 Juni, wakati kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 93 alipoondoka kwenda Uswisi kwa ajili ya kile ambacho maafisa walikitaja kuwa "ziara fupi ya binafsi" akiwa na mkewe, Chantal.
Biya, ambaye aliingia madarakani mwaka 1982 baada ya kuhudumu kama Waziri Mkuu kwa miaka saba, amekuwa akiondoka Cameroon kwa vipindi virefu zaidi katika miaka ya hivi karibuni, huku akitumia muda mwingi katika hoteli ya nyota tano ya InterContinental jijini Geneva.





