Rais Ruto akataa kupitisha Muswada wa Fedha 2024.
Eric Buyanza
June 26, 2024
Share :
Rais wa Kenya William Ruto amekataa kutia saini Muswada wa Fedha wa 2024 uliopitishwa na bunge siku ya jana.
Taarifa iliyotolewa na Chombo cha habari cha Kenya Star kimeripoti kuwa vyanzo vya habari vya Ikulu kuwa Muswada huo utarejeshwa Bungeni kabla ya mapumziko ya leo Juni 26.
Mkuu huyo wa Nchi amependekeza marekebisho ya Mswada huo ulioidhinishwa siku ya jana na zaidi ya nusu ya wabunge.
Hata hivyo, taarifa nyingine kutoka Nchini humo zinasema Rais Ruto anatarajia kuhutubia Nchi leo jumatano saa 10 jioni.