pmbet

Rais Ruto asalimu amri kwa waandamanaji akubali mazungumzo.

Joyce Shedrack

June 24, 2024
Share :

Rais wa Kenya Dkt. William Ruto amekubali kufanya mazungumzo na waandamanaji kufuatia maandamano yaliyokuwa yanaendelea Nchini humo yakiongozwa na kundi la vijana wenye umri mdogo.

Akizungumza akiwa kwenye Kanisa moja lililopo Mji wa Nyahururu Nchini humo Dkt. Ruto amesema amesema yuko tayari kufanya mazungumzo na maelfu ya Vijana waliofanya maandamano ya amani wiki iliyopita kote Nchini huku akiwapongeza Vijana hao kwa kujitokeza na kushughulika na mambo ya Taifa lao.

“Ninajivunia sana Vijana wetu, wamepiga hatua mbele kwa kufanya maandamano ya amani na ninataka kuwaambia kwamba tutafanya mazungumzo na nyie ili tuweze kusikiliza mambo yenu na kwa pamoja tulijenge Tifa letu". Amesema Dkt. Ruto.

Maandamano hayo yalifanyika wiki iliyopita kwenye miji mbalimbali Nchini Kenya huku kundi kubwa la washiriki likiwa ni Vijana Wakenya wengi wenye umri mdogo waliokuwa wakishinikiza kutoridhika na sera za kiuchumi za Serikali ya Nchi yao.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet