pmbet

Rais Ruto asikitishwa na mauwaji ya waandamanaji siku ya jana.

Eric Buyanza

June 26, 2024
Share :

Rais wa Kenya William Ruto amehutubia Taifa leo kwa mara ya pili tangu kuanza kwa maandamano Nchini humo ya kupinga Muswada wa Fedha wa mwaka 2024.

 

Kupitia hotuba hiyo Rais Ruto amesema alichukua Nchi miezi nane iliyopita ikiwa na madeni makubwa hivyo lengo la kuongeza kodi ilikuwa ni ili kuweza kulipa madeni aliyoyakuta lakini ameamua kusikiliza sauti za Wakenya na kukubali kutosaini Muswada huo wa Fedha na badala yake  watapunguza matumizi katika Ofisi ya Rais ili kulipa madeni ya Serikali.

 

Yafuatayo ni mambo 10 ya muhimu aliyoyazungumza Rais Ruto kwenye hotuba yake……….

*Nakubali kwamba sitasaini Muswada wa Fedha 2024, na nimeuondoa.
*Nataka kuwashukuru wabunge waliopiga kura ya 'Ndiyo' kwa muswada kubainisha kipaumbele cha taifa letu.
*Nilipotoa mapendekezo ya Bunge tulikuwa na vipaumbele muhimu kwa taifa letu.
*Muswada huo ulikua unalenga kuboresha sekta ya elimu na afya, haswa wenye maradhi ya saratani na kisukari. 
*Sera za kupunguza bei ya bidhaa muhimu zimefanya kazi.
*Nafanya juu chini kuhakisha tumepunguza deni linalokumba taifa hilo.
*Tumelipa deni ya dola bilioni 2 ya Eurobond. Ni funzo kwa taifa kujua kwamba kwa kila shilingi 100 tunayokusanya kama ushuru sisi hutuma shilingi 60 katika kulipa deni. 
*Ninaelekeza hatua zaidi za kubana matumizi ili kupunguza matumizi katika ofisi ya rais na urais wote na kuenea kwa kitengo kizima cha serikali. 
*Watu waliotekwa nyara na polisi wote wamepatikana gerezani, hakuna aliyeuawa.
*Najutia matukio ya jana yaliosababisha kuuliwa kwa waandamanaji.

 

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet