pmbet

Rais Samia aahidi kuongeza miundombinu Mbeya

Sisti Herman

September 4, 2025
Share :

 

Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kuendelea kuwekeza kwenye sekta za kilimo, mifugo na miundombinu kama uti wa mgongo wa uchumi wa wananchi wa Mbeya na taifa kwa ujumla.

Akizungumza Septemba 4, 2025, katika mkutano wa kampeni uliofanyika Mbalizi, mkoani Mbeya, Dkt. Samia amesema kuwa zaidi ya asilimia 85 ya wakazi wa eneo hilo ni wakulima, na serikali yake imejipanga kuhakikisha wanawezeshwa kwa pembejeo, ruzuku na huduma bora za ugani.

“Tuliwasikia kilio chenu cha mbolea, tangu 2022 nilipozungumza nanyi. Leo hii mbolea ya ruzuku inapatikana siyo tu Mbeya, bali nchi nzima. Tumeboresha zaidi kwa kuweka mbolea mahsusi kwa kila zao: mahindi, mpunga, parachichi na mengine. Lengo letu ni Tanzania kujilisha na kuuza ziada kwa majirani zetu,” amesema Dkt. Samia.

Aidha, ametoa wito kwa wakulima kuendelea kujisajili na kutunza namba zao za siri ili kufanikisha upatikanaji wa ruzuku, huku akisisitiza kuwa pembejeo hizo hazipaswi kuuzwa kwa nia ya biashara, bali kutumika kuzalisha chakula na mazao ya biashara.

Akizungumzia sekta ya mifugo, Dkt. Samia amesema serikali inakamilisha ujenzi wa machinjio ya kisasa katika eneo la Utengule, ambayo italeta mapinduzi katika biashara ya nyama na mifugo.

“Tunataka nyama na wanyama wetu wawe na hadhi ya kuuzwa nje ya nchi bila maswali. Ndiyo maana tumeanzisha kampeni ya chanjo na utambuzi wa mifugo. Wafugaji endeleeni kufuga, fursa ya kuuza nyama na wanyama hai kimataifa ni kubwa,” amesema.

Dkt. Samia pia ameahidi kuendelea na ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja ili kuwezesha usafirishaji wa bidhaa za kilimo na mifugo kutoka mashambani hadi sokoni.

“Ahadi yangu ni kuhakikisha barabara zote zilizo kwenye ilani ya CCM zinajengwa. Wakandarasi tayari wapo kazini na tutajenga madaraja yote bila kujali ukubwa wake. Miundombinu hii ndiyo itakayorahisisha biashara na kuongeza kipato cha wananchi,” ameongeza.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet