Rais Samia aahidi uchaguzi mkuu wa huru na haki - Kinana
Eric Buyanza
March 6, 2024
Share :
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana amewahakikishia watanzania kwamba Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu na Uchaguzi Mkuu mwakani utakuwa wa huru na wa haki.
Amesema dhamira ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha mchakato wa uchaguzi unakuwa huru na wa haki ili watu wapate fursa ya kuchagua viongozi wanaowataka.