pmbet

Rais Samia agharamia safari ya Simba kwenda Afrika Kusini.

Joyce Shedrack

April 23, 2025
Share :

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameiunga mkono klabu ya Simba kwa kulipia gharama za kwenda Afrika Kusini pamoja na malazi kwa timu hiyo katika kipindi chote itakapokuwa huko kwa ajili ya mchezo wa marudiano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Stellenbosch, Aprili 27, 2025.

Rais wa Heshima na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Mohammed Dewji amethibitisha taarifa hiyo huku akitoa shukrani kwa Rais Samia kwa niaba ya klabu ya Simba.

“Kwa niaba ya Klabu ya Simba Sports Club, napenda kutoa shukrani za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwa kuiwezesha klabu yetu kushiriki mashindano ya kimataifa".

“Tumepokea kwa moyo wa shukrani mchango wa malazi na usafiri kwa ajili ya mchezo wetu wa marudiano wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Stellenbosch".

“Klabu ya Simba inatambua na kuthamini kwa dhati juhudi za Rais Samia katika kumarisha sekta ya michezo hapa nchini, hususan mpira wa miguu,” imesema barua aliyoandika Mohamed Dewji.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet