Rais Samia aidhinisha oktoba 29 kuwa siku ya mapumziko.
Joyce Shedrack
October 24, 2025
Share :
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan, kwa kutumia mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya Sikukuu
za Kitaifa Sura 35, ameidhinisha tarehe 29 Oktoba, 2025 kuwa siku ya mapumziko.

Dkt.Samia amefanya uamuzi huo kwa madhumuni ya kuwawezesha wananchi wenye sifa stahiki wakiwemo watumishi wa umma na wafanyakazi katika sekta binafsi kutumia haki yao ya kikatiba ya kupiga kura.





