Rais Samia aipongeza Simba kushinda 6-0 CAF
Sisti Herman
March 2, 2024
Share :
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewapongeza klabu ya Simba baada ya ushindi wa kishindo wa goli 6-0 dhidi ya Jwaneng' Galaxy kwenye mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika ambao umewapeleka Simba robo fainali ya michuano hiyo.
“Hongereni sana Klabu ya Simba kwa kufanikiwa kufuzu hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Mafanikio yenu si tu furaha na fahari kwa mashabiki na wanachama wa Klabu ya Simba, bali pia kwa Taifa na Watanzania wote.”- Rais wa Tanzania, Dkt.
Mabao ya Simba kwenye mchezo huo walioubatiza wa kisasi cha misimu miwili iliyopita kwa kufungwa 3-0 na kuondoshwa kwenye hatua za awali ya michuano hiyo yalifungwa na Saido Ntibanzokiza, Par Omar Jobe, Kibu Denis, Clatous Chama, Ladack Chasambi na Fabrice Ngoma.
Simba inaungana na Yanga kwenye robo fainali huku Tanzania ikiwa nchi pekee Afrika kupeleka timu 2 kwenye hatua hiyo.