pmbet

Rais Samia aipongeza Yanga kufuzu Robo fainali CAF

Sisti Herman

February 25, 2024
Share :

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameipongeza klabu ya Yanga kwa kufuzu robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika kwa mara ya kwanza kwenye historia yao baada ya kuwachapa CR Belouizdad 4-1 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jana.

 

“Naipongeza Klabu ya Yanga kwa kufanya vyema katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), na kufanikiwa kufuzu hatua ya Robo Fainali. Mafanikio haya yameandika historia kubwa kwa klabu na sekta ya michezo nchini. Mmeleta furaha kwa mamilioni ya mashabiki wenu na Watanzania kwa ujumla” aliandika Dkt. Samia kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet