pmbet

Rais Samia aitisha kikao maalum kujadili Maafa na Muungano

Sisti Herman

April 14, 2024
Share :

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan jana ameongoza kikao maalum kilichowasilisha ripoti ya maafa ya Mafuriko yaliotokea sehemu mbalimbali nchini ikiwemo Rufiji, Morogoro, Lindi na Arusha.

Viongozi wakubwa waliohudhuria kikao hicho ni pamoja na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, Naibu Waziri Mkuu Mhe. Dotto Biteko,Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na viongozi wengine wa Serikali.

Vile vile, kamati maalum imewasilisha maandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ikulu ndogo ya Tunguu Zanzibar tarehe 13, Aprili 2024.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet