Rais Samia akutana na Rais wa Korea Kusini
Sisti Herman
June 2, 2024
Share :
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 02 Juni, 2024 akiwa kwenye ziara rasmi nchini Korea Kusini amekutana Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Korea Mhe. Yoon Suk Yeol katika Ikulu ya Nchi hiyo iliyopo Seoul kwa ajili ya mazungumzo na kushuhudia hafla ya utiaji saini Mikataba mbalimbali
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo Rasmi na Rais wa Jamhuri ya Korea Mhe. Yoon Suk Yeol ikiwa ni pamoja na kushuhudia utiaji saini wa mikataba mbalimbali.