pmbet

Rais Samia Amlilia Papa Francis.

Joyce Shedrack

April 21, 2025
Share :

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesikitishwa na kifo cha kiongozi wa Waumini wa Dini ya kikatoliki kufuatia kifo cha Papa Francis aliyefariki Dunia leo April 21, 2025 huko Vatican.

Pope Francis' Easter is going to look a little different this year. Here's  how | CNN

Kupitia ukurasa wake rasmi kwa niaba ya Serikali Rais Samia ametoa salamu za pole kwa Waumini wa dini hiyo kufuatia Kifo cha Papa Francis.

 

Kupitia mtandao wake wa Instagram Rais Dkt @samia_suluhu_hassan ameandika "Nimesikitishwa na taarifa ya kifo cha Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francisko.

 

Katika kipindi chote cha miaka 12 akiwa Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francisko ameishi maisha yake kama mwalimu na kiongozi aliyefundisha na kuhimiza ustawi na maendeleo ya watu pamoja na kudumisha amani.

 

Kwa niaba ya Serikali na Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ninatuma salamu za pole kwa waumini wote wa Kanisa Katoliki hapa nchini na duniani kote. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet