Rais Samia amteua Masaju kuwa Jaji Mkuu, kumrithi Prof Ibrahim
Eric Buyanza
June 13, 2025
Share :
#UTEUZI Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Jaji wa Mahakama ya Rufani, George Masaju kuwa Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania.
Jaji Masaju anachukua nafasi ya Jaji Profesa Ibrahim Juma ambaye amestaafu rasmi.
Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu kwa vyombo vya habari leo Ijumaa, Juni 13, 2025, Jaji Masaju ataapishwa Juni 15, 2025 katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.