pmbet

Rais Samia aomboleza kifo cha Rais Namibia

Sisti Herman

February 4, 2024
Share :

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameungana na Watanzania wote kuomboleza na kutoa pole kwa wananchi wa Namibia kufuatia kifo cha Rais wa Namibia Hage Geingob ambaye amefariki dunia leo Feb 04,2024 wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Lady Pohamba iliyopo Mji Mkuu wa Nchi hiyo Windhoek, Ofisi ya Rais wa Namibia imethibitisha taarifa hiyo na kusema amefariki wakati Mkewe Monica Geingos na Mwanae wakiwa karibu nae.

"Nimehuzunishwa sana na kifo cha Rais wa Namibia, Mheshimiwa Hage Geingob, ndugu mpendwa, mwana Pan Africanist na rafiki mkubwa wa Tanzania. Kwa niaba ya wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, natuma salamu za rambirambi kwa wananchi wa Jamhuri ya Namibia, Kaimu Rais, Mheshimiwa Dkt. Nangolo Mbumba, Mke wa Rais, Mheshimiwa Monica Kalondo, familia, marafiki na wandugu. katika SWAPO. Ninyi nyote mfarijike katika kipindi hiki kigumu. Roho yake ipumzike kwa amani. Amina" aliandika Rais Samia kupitia mitandao yake ya kijamii

Rais huyo mwenye umri wa miaka 82 aligunduliwa kuwa anaugua saratani na alitangaza hali yake mbele ya umma mwezi uliopita na baadaye ofisi yake ilitangaza kwamba atasafiri kuelekea Marekani kupata matibabu, itakumbukwa pia alifanyiwa upasuaji wa moyo mwaka jana, na mwaka 2014 alitangaza kuwa amepona saratani ya tezi dume.

Geingob aliapishwa kuwa Rais mwaka 2015 na alikuwa anatumikia awamu yake ya pili na ya mwisho ya uongozi.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet