Rais Samia aongoza kikao cha Kamati kuu CCM
Sisti Herman
September 1, 2024
Share :
Kikao Maalum cha Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana leo September 01, 2024 ambacho kimongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kimewaondoa Viongozi watatu wa Chama hicho kwenye nafasi zao kwa kukiuka maadili ya uongozi.
Taarifa iliyolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Gabriel Makalla imesema walioondolewa ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania, Jumuiya ya CCM Mkoa wa Lindi, Palina Ninje, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani Abdul Rashid Zahoro na Munira George Nkango ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Singida.
Katika hatua nyingine Kamati Kuu imefanya uteuzi wa majina ya Wana-CCM 10 kugombea nafasi ya ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), kati ya Wanachama 47 walijitokeza kuwania uteuzi huo, walioteuliwa na Kamati Kuu ni Gladness Salema, Maria Alphonce, Queenelizabeth Makune, Ester Chaula, Prof. Neema Kumburu, Lucia Pande, Fatuma Kange, Hawa Mkwela, Fatma Msofe na Theresia Dominic.
“Wagombea walioteuliwa, watapigiwa kura kesho Jumatatu, September 2, 2024 na kikao cha Kamati ya Wabunge wa CCM, saa 8 mchana, Jijini Dodoma kisha September 5 2024, kutakuwa na uchaguzi wa kumpata Mbunge mmoja kwa kuchaguliwa na Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”