Rais Samia apunguzia gharama za matibabu kwa wananchi wa Kagera
Eric Buyanza
June 18, 2024
Share :
Mkuu wa wilaya ya Bukoba Mhe Erasto Sima ambae amemuwakisha Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe Hajat Fatuma Mwassa kuwapokea madaktari Bingwa arobaini (40) marufu kama Madaktari Bingwa wa Mama samia hafla hiyo iliyofanyika katika Hospitali ya manispaa ya Bukoba. Ambapo Madaktari Bingwa wa Mama Samia Suluhu Hasani watakaotoa huduma za kibingwa katika Hospitali za Halimashauri nane za Mkoa wa Kagera.
Mhe.Erasto Sima wakati wa kuwapokea Madaktari Bingwa wa Mama Samia amesema " Kipekee kabisa ninapenda kuishukru Serikali ya awamu ya Sita Inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kuboresha huduma za Afya kwa wananchi wa mkoa wa Kagera kwa kuhakikisha wanapata huduma bora za Afya na kwa gharama nafuu.
Aidha ninapenda kuishukru serikali ya awamu ya sita kuoitia wizara ya Afya na TAMISEMI kwa kuratibu zoezi hili la Madaktari Bingwa wa Mama Samia ambao wanakwenda kuwapunguzia wananchi gharama za matibabu za kibingwa ambazo wangezipata mbali ila kuoitia hii programu ya Madaktari wa Mama Samia wananchi wanakwenda kupata huduma karibu na kwa gharama nafuu "DC Sima"
Hivyo basi nitoe wito kwa wananchi wote wenye matatizo ya magonjwa na wenye uhitaji wa kufanyiwa uchunguzi na matibabu ya kibingwakufika kwenye eneo la Hospitali za wilaya zilizopo mkoani Kagera kuanzia leo tarehe 17 Juni, hadi 21 Juni 2024."
Mwisho Mganga mkuu wa Mkoa wa Kagera Dkt Samwel Laizer amesema " Sisi kama wasimamizi wa Huduma za Afya kwenye Mkoa wa Kagera tunamshukru sana Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea Madaktri Bingwa ambao wanakwenda kutoa huduma kwa wananchi na pia kuwajengea uwezo watumishi waliopo katika vituo vyetu vya kutolea Huduma, haya ni mafanikio makubwa ambayo Serikali ya awamu ya Sita chini ya Dkt. Samia Mageuzi makubwa ya ubora wa huduma yamefanyika na yanaonekana, Sisi pamoja na timu yangu tutahakikisha Madaktari Bingwa wote mliokuja kutoa huduma kwenye mkoa wa Kagera tunawapa ushirikiano wa kutosha".