Rais Samia asherekea siku ya mtoto wa Afrika na watoto Ikulu.
Sisti Herman
June 16, 2024
Share :
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akisherehekea Siku ya Mtoto wa Afrika akiwa pamoja na wajukuu, Ikulu jijini Dar es Salaam. Siku hii huadhimishwa Juni 16 ya kila mwaka.
Katika kuadhimisha siku hii, Rais Samia amesisitiza umuhimu wa Serikali, familia na jamii kushirikiana kuhakikisha watoto wanapata malezi bora yenye maadili mema, na kuhakikisha usalama wa mtoto ni jukumu la jamii nzima na siyo mzazi tu, vilevile kuwapatia elimu na historia za kuwahimiza uzalendo kwa nchi yao tangu wakiwa wadogo.