Rais Samia asikitishwa kifo cha Dida atoa pole.
Joyce Shedrack
October 5, 2024
Share :
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa salamu za pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wafanyakazi wa Wasafi Media Group kufuatia kifo cha aliyekuwa Mtangazaji wa Kipindi cha Mashamsham cha Wasafi FM Khadija Shaibu (Dida) aliyefariki dunia jana Oktoba 4, 2024 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa Matibabu.
Rais Samia ametoa pole hizo huku akionyesha kusikitishwa na msiba huo kupitia taarifa aliyoitoa kwenye ukurasa wake wa Instagram.
"Ninatoa salamu za pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wafanyakazi wa Wasafi Media Group kwa kuondokewa na ndugu yetu, Khadija Shaibu (Dida). Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma awape subra.
Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un.
Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwa hakika kwake Yeye tutarejea." ameandika Rais Samia.