Rais Samia atekeleza ujenzi wa mradi mkubwa wa maji Makonde.
Joyce Shedrack
December 4, 2024
Share :
Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ametekeleza ujenzi wa mradi mkubwa wa maji Makonde utakaohudumia halmashauri nne.
Mradi wa maji Makonde umegharimu shilingi bilioni 84.7 za Kitanzania ukitarajiwa kumaliza kabisa changamoto za upungufu na ukosefu wa maji kwa wakazi wa Newala, Tandahimba na Nanyamba.