pmbet

Rais Samia atengua Uteuzi wa Vigogo TTCL na Posta

Sisti Herman

July 23, 2024
Share :

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Viongozi mbalimbali akiwemo Zuhura Sinare Muro, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na Mhandisi Peter Rudolph Ulanga, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).

Rais amemtengua pia uteuzi wa Brigedia Jenerali Mstaafu Yohana Ocholla Mabongo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Tanzania na Maharage Aly Chande, Postamasta Mkuu, Shirika la Posta Tanzania.

Wengine ambao Uteuzi wao umenguliwa ni Prof. John Nkoma, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (USAF) na Justina Tumaini Mashiba, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF).

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet