Rais Samia ateua K/Mkuu mpya Wizara ya Nishati
Sisti Herman
February 21, 2024
Share :
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Dr. James Peter Mataragio kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati akichukua nafasi ya Athumani Selemani Mbuttuka ambaye uteuzi wake umetenguliwa na atapangiwa kazi nyingine.
Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu imeeleza kuwa Dr. Mataragio aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania.