Rais Samia atunukiwa Shahada ya Heshima (SUZA)
Eric Buyanza
December 28, 2023
Share :
Rais Samia Suluhu Hassan leo Desemba 28, 2023, ametunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu ya Usimamizi wa Utalii na Masoko katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA).
Chuo hicho kimemtunuku Shahada hiyo kwa kutambua mchango wake wa kuifungua nchi kiuchumi kupitia sekta ya utalii.