pmbet

Rais Samia awaambia Katavi "Mtaachana na majenereta Septemba"

Eric Buyanza

July 13, 2024
Share :

Rais Samia Suluhu Hassan amewaahidi wananchi wa Wilaya ya Mlele mkoani Katavi kuwa hadi kufikia mwezi Septemba mwaka huu wilaya hiyo itaunganishwa na umeme wa gridi ya Taifa na hivyo kuachana na adha ya matumizi ya Jenereta.

Amesema majenereta yamekuwa yakitumia fedha nyingi ili kuzalisha umeme akitaja kiasi cha shilingi milioni 2 na zaidi kimekuwa kikitumika kwa mwezi mmoja katika mkoa huo.

Amesema hayo wakati akizungumza na wananchi hao katika viwanja vya Shule ya Msingi Inyonga. Rais yuko katika ziara ya kikazi mkoani Katavi. 

Aidha Rais Samia ametoa wito kwa wananchi kufanya matumizi ya umeme huo kwa maslahi ya kiuchumi.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet