Rais Samia awaapisha viongozi wa Tume ya Kurekebisha Sheria
Sisti Herman
April 28, 2024
Share :
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo ameongoza hafla fupi ya kuwaapisha viongozi wa Tume ya kurekebisha sheria Ikulu jijini Dar es Salaam.
Walioapishwa katika hafla hiyo ambayo pia imehudhuriwa na Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Munngano wa Tanzania Mussa Azan 'Zungu' na Jaji Mkuu wa Mahakama Prof. Ibrahim Hamis Juma, ni Ndugu Bibiana Joseph Kileo Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka, Ndugu Alice Edward Mtulo Naibu Wakili Mkuu wa Serikali na Ndugu Winfrida Beatrice Korosso Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania
Picha juu (kwa hisani ya Ikulu) ni viongozi wa Tume walioapishwa pamoja na viongozi Wakuu wa Serikali, Bunge na Mahakama mara baada ya hafla fupi ya kuwaapisha iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Aprili, 2024.