Rais Samia awaapisha Wajumbe wa Tume ya mipango
Sisti Herman
May 29, 2024
Share :
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 29 Mei 2024 amewaapisha na kuzungumza na Wajumbe wa Tume ya Mipango katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
Miongoni mwa walioapishwa ni Waziri wa fedha Mhe. Dkt Mwigulu Issack Nchemba, Waziri wa mipango na uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo, Balozi Ombeni Sefue, Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, Balozi Ami Ramadhan Mpungwe.
Lengo la Tume hii ni kusimamia uchumi, mchakato wa upangaji na utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Taifa.