Rais Samia azindua kanisa jipya la Mwamposa.
Joyce Shedrack
July 5, 2025
Share :
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua rasmi mahema mapya ya Kanisa la Arise and Shine lililopo Kawe Jijini Dar es salaam.
Mpaka kukamilika kwa ujenzi wa awamu ya pili wa Kanisa la Arise and Shine, zaidi ya TZS bilioni 15 zimetumika.
Taarifa ya kanisa hilo imeeleza kuwa fedha hizo ni sadaka pamoja na shughuli mbalimbali za kanisa hilo linalokadiriwa kuwa na uwezo wa kuchukua takribani waumini 50,000.