Rais Samia kuzindua benki ya kuhifadhi mbegu za uzazi
Eric Buyanza
February 29, 2024
Share :
Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua benki ya kuhifadhi mbegu za uzazi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili hivi karibuni.
Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel amesema MNH imeanza kuhifadhi mbegu hizo za uzazi na mtu akitaka kupata mtoto basi atafika hospitalini hapo na kupandikiziwa.
“Mbegu zitahifadhiwa kwa muda wa miaka mitano hadi 10, mtu kama hahitaji mtoto kwa wakati husika zitahifadhiwa, wakati akiona sasa anahitaji kupata mtoto basi atapandikiziwa,” amesema.
“Sio lazima uende Uturuki kupandikiza mimba, Muhimbili tunafanya na kama ukihitaji kuhifadhi mayai yako hutaki mtoto kwa sasa hadi hapo baadae tunakuhifadhia mayai yako hadi hapo baadae utakapokuwa tayari tutalikutanisha na kupata mtoto,” amesema Dk Mollel .